Mnigeria akamatwa JNIA kwa kupatikana na cocaine

Polisi Kikosi cha Viwanja vya Ndege jijini Dar es Salaam linamshikilia raia wa Nigeria akituhumiwa kupatikana na dawa za kulevya aina ya Cocaine.

Christian Ugbechi (26), anadaiwa kukamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa kwa Julius Nyerere (JNIA) akiwa na pipi 59 zenye uzito wa zaidi gramu 800.

Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, Matanga Mbushi amesema leo Jumatatu Januari 29,2018 kuwa mtuhumiwa anaishi na kufanya kazi nchini Ufaransa.

Amesema alikuwa akisafirisha dawa hizo za kulevya kwenda nchini Ufaransa.

"Tumemkamata mtuhumiwa akiwa na pipi 59, kati ya hizo 56 alizificha kwenye soksi na tatu amezitoa leo kwa njia ya haja kubwa. Yupo chini ya uangalizi maalumu,” amesema Mbushi.


from MPEKUZI

Comments