Kigwangalla aagiza polisi kuwakamata vigogo wanne, la sivyo atafikisha taarifa kwa Rais Magufuli

Waziri wa Maliasili na utalii Dkt.Hamis Kigwangala amelitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha linawakamata watu wanne waliopanga mauaji ya mhamasishaji wa utalii Wayne Lotter mwaka Jana jijini Dar es Salaam la sivyo atafikisha taarifa hiyo kwa Rais John Magufuli.

Dkt. Kigwangalla amesema kuwa watu hao waliopanga kufanyika mauaji hayo ni vigogo wapo wanne na wanajulikana.

"Ninawajua viongozi wanne ambao ni vigogo kuwa wameshiriki katika kupanga mauaji ya mhamasishaji wa utalii nchini Wayne Lotter," alisema Dkt Kigwangalla

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo Januari 25, 2018 na kusisitiza kuwa katika kipindi cha siku 100, wizara yake imebaini mitandao 74 ya watu wanaojihusisha na ujangili ikiwa na washiriki 949.

Amesema kati ya watu hao, 949 tayari wamefikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili huku wengine wakisubiri kufikishwa mahakamani.



from MPEKUZI

Comments