Mahakama Yatoa Uamuzi Kesi ya Akina Mdee Kupinga Kufukuzwa Uanachama Chadema


Mahakama Kuu imewaruhusu waliokuwa wanachama wa Chadema, Halma Mdee na wenzake 18 kufungua shauri la kupinga uamuzi wa chama hicho kuwavua uanachama.

Mahakama hiyo imetoa ruhusa hiyo kwa kina Mdee leo Ijumaa Julai 8, 2022, baada ya kukubaliana na hoja za maombi yao ya ridhaa ya kufungua shauri hilo la kupinga kuvuliwa uanachama.

Maombi hayo ya kina Mdee yalisikilizwa na Jaji Mustapha Ismail Juni 30 mwaka huu na Chadema kupitia kwa jopo la mawakili wao linaloongozwa na Peter Kibatala, walipinga hoja za mawakili wa kina Mdee kuwa hazikidhi matakwa ya kisheria kupewa ruhusa hiyo

Hata hivyo Jaji Ismail katika uamuzi wake leo amekubaliana na vigezo na hoja zote za kina Mdee, zilizowasilishwa na mawakili wao, Ipilinga Panya, Aliko Mwamanenge, Edson Kilatu na Emmanuel Ukashu.

Kwa uamuzi huo sasa kina Mdee wanatakiwa kufungua shauri lao hilo ndani ya siku 14 kuanzia leo.


from MPEKUZI

Comments