Biden asema Marekani itatumia "nguvu zake zote" kuizuia Iran kupata silaha za nyuklia


Rais wa Marekani Joe Biden ameahidi leo kuwa nchi yake itatumia "nguvu zote ilizo nazo" kuizuia Iran kumiliki silaha za nyuklia. 
 
Biden ametoa ahadi hiyo baada ya kujiunga na waziri mkuu wa Israel Yair Lapid mjini Jerusalem kutia saini mkataba wa ushirikiano unaosisitiza nia ya Marekani ya kuendelea kuisaidia Israel kujilinda dhidi ya kile kinatajwa kuwa kitisho kwa dola hiyo ya kiyahudi.Waziri mkuu wa Israel ameusifu mkataba huo mpya na dhamira iliyoelezwa na Biden.
 
Chini ya mkataba huo uliosainiwa wakati wa siku ya pili ya ziara ya Biden nchini Israel, Marekani pia inatoa hakikisho la kuyakabili makundi ya wanamgambo yenye mafungamano na Tehran.


from MPEKUZI

Comments