OR-TAMISEMI yatoa mwongozo kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano kubadilisha shule,tahasusi


KAIMU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dkt. Charles Msonde amesema wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano kwenye maeneo mbalimbali na wana changamoto za ugonjwa ama walikosea kujaza Selfom kwa kuandika maeneo ya kuishi tofauti na uhalisia kuwasilisha changamoto hizo kwa Makatibu Tawala wa Mikoa yao ili ziweze kutatuliwa.

Dkt. Msonde ameyasema hayo leo wakati akitoa taarifa ya maandalizi ya kufungua shule wa wanafunzi wa Kidato cha Tano Juni 13,222.

Amesema, kufuatia taarifa iliyotolewa na Waziri wa Nchi-TAMISEMI, Mhe.Innocent Bashungwa mnamo Mei 13,2022 ya kuwapangia shule wanafunzi wa Kidato cha tano na vyuo Ofisi ya Rais-TAMISEMI imekuwa ikipokea maombi kutoka kwa wazazi ama wanafunzi wenyewe ya kubadilisha shule au tahasusi kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za ugonjwa, kukosea ujazaji wa Selform kwa kuonyesha maeneo ya kuishi tofauti na uhalisia. 

"OR-TAMISEMI inasisitiza kwa wale wote wenye changamoto hizo waziwasilishe kwenye ofisi za Makatibu Tawala wa Mikoa ili zitatuliwe. 

"Makatibu Tawala wa Mikoa wameshapatiwa mwongozo wa namna ya kushughulikia changamoto za uhamisho na ubadilishaji wa tahasusi ili wautumie kama rejea wakati wa kushughulikia changamoto mbalimbali za wazazi na wanafunzi," amesema.

Pia amebainisha kuwa, wanafunzi walichaguliwa na kupangiwa shule kwa kuzingatia machaguo yao waliyopendekeza na ushindani miongoni mwao katika machaguo hayo pamoja na shule walizopendekeza. 

Aidha, idadi ya wanafunzi waliopangiwa kwenye kila shule ilitegemea na nafasi zilizokuwepo katika kila shule ili kuepusha msongamano kwa wanafunzi darasani na mahali pakulala.  

Pia amewataka wanafunzi hao kuhakikisha wanatipoti shuleni si zaidi ya wiki mbali tangu tarehe ya kufungua shule ambayo ni Juni 13,2022 kinyume na hapo nafasi hiyo itapewa mwanafunzi mwingine ambaye yuko kwenye orodha ya kusubiria.



from MPEKUZI

Comments