Miradi ya kimkakati kuendelea kukamilishwa 2022/2023


Serikali imesema katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 itaendelea kukamilisha miradi ya kielelezo na ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini, ambayo inatarajiwa kuwa na matokeo mapama ya haraka katika uchumi wa Taifa.

  Kauli hiyo ya Serikali imetolewa bungeni jijini Dodoma na Waziri Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba wakati akiwasilisha Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2021 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.
Amesema miradi hiyo ya kielelezo na ya kimkakati inatarajiwa kuzalisha ajira, kuongeza kipato pamoja na kupunguza hali ya umaskini nchini.

  Dkt. Mchema ameitaja miradi hiyo kuwa pamoja na ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (SGR), mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere, kuboresha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) na mradi wa kuchakata na kusindika gesi asilia kuwa kimiminika (LNG) huko mkoani Lindi.

  Waziri huyo wa Fedha na Mipango ameongeza kuwa miradi ya kipaumbele kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 itaendelea kuzingatia maeneo matano ya kipaumbele ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano kuanzia mwaka 2021/2022 hadi 2025/2026.




from MPEKUZI

Comments