Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua Filamu ya Tanzania: Royal Tour kitaifa katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Uzinduzi wa filamu hiyo ulianzia Marekani katika miji miwili ya New York na Los Angeles Aprili 18 na 21, 2022 ikafuatia Tanzania ambapo Arusha ilizinduliwa Aprili 28 ikifuatia Zanzibar Mei 7 na kuhitimishwa Kitaifa jijini Dar es Salaam Mei 8, 2022
Filamu hiyo imelenga kutangaza vivutio vya Utalii nchini Tanzania
“Tuliona utalii wa Tanzania unaterereka yaani umekuwa laini sana, sasa kutokana na mwenendo huo wa kupanda na kushuka tukaona njia nzuri ni kuutangaza kimataifa na filamu hii imetangaza mazingira ya misitu ya Tanzania” Rais Samia Suluhu Hassan
Aidha Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya Royal Tour Dkt. Hassan Abbas amesema baada ya uzinduzi wa Filamu hiyo vituo vya televisheni vya ndani vitakuwa na haki ya kuonyesha filamu hiyo.
“Leo baada tu ya kuzinduliwa sasa vituo vyote vya televisheni vya ndani vitakuwa na haki ya kuicheza filamu hii kadri iwezekanavyo kuanzia” Dkt Hassan Abbas
Uzinduzi huo umeshuhudiwa na viongozi wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwepo Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, Rais wa Zanzibar Dkt. Hussen Mwinyi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment