Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson Apigwa Marufuku Kuingia Urusi


KWA mara ya kwanza tangu vita kati ya Urusi na Ukraine ianze Urusi imetamka rasmi kupitia kwa Waziri wake wa Mambo ya Nje kumpiga marufuku Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson kukanyaga katika ardhi ya Urusi yeye pamoja na Mawaziri wengine kumi na mbili.

Sambamba na Boris, Urusi imempiga marufuku Katibu wa Wizara ya Mambo ya Nje Liz Truss, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi Ben Wallace pamoja na wafanyakazi wengine 10 wa Serikali ya Uingereza kutoingia nchini Urusi.

Viongozi wengine wa Uingereza waliopigwa marufuku kuingia nchini Urusi ni Dominic Raab, Grant Shapps, Priti Patel, Rishi Sunak, Kwasi Kwarteng, Nadine Dorries, James Heappey, Nicola Sturgeon, Suela Braverman pamoja na Thereza May.


from MPEKUZI

Comments