Maunda Zorro Afariki Dunia kwa Ajali ya Gari


Msanii  wa Bongofleva, Maunda Zorro amefariki dunia kwa ajali ya gari, usiku wa kuamkia leo, April 14, 2022 baada ya gari alilokuwa amepanda aina ya VITZ kugongana uso kwa uso na lori la mchanga Kigamboni, Dar es Salaam.

Kaka wa marehemu ambaye pia ni msanii wa Bongofleva, Banana Zorro  ametoa taarifa ya kinachondelea kuhusu msiba wa Maunda Zorro kwa kueleza kwamba kwa sasa msiba upo Maweni Kigamboni kwa Mzee Zorro na taarifa zaidi kuhusu msiba huo zitatolewa baadaye.



from MPEKUZI

Comments