Spika wa Bunge, Dk Tulia Akson ameahirisha kikao cha Bunge leo Jumatatu Aprili 25, 2022 kufuatia kifo cha Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Rukwa (CCM), Irene Ndyamkama kilichotokea jana katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha alikokuwa akipatiwa matibabu.
Dk Tulia amesema mwili wa mbunge huyo unatarajia kuagwa na wabunge Jumatano Aprili 27, 2022 katika viwanja vya bunge jijini Dodoma.
Kanuni za bunge zinaelekeza unapotokea msiba wakati wa vikao vya bunge, shughuli za siku hiyo zitaahirishwa kwa ajili ya kutoa nafasi kwa wabunge kufanya maombolezo.
Spika amesema taratibu zingine kuhusu ratiba nzima zitatangazwa kwa wabunge kadri watakavyojadiliana na familia.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment