Wahouthi wafanya mfululizo wa mashambulizi dhidi ya Saudi Arabia


Waasi wa Kihouthi wamefanya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani na makombora katika vituo muhimu vya nishati vya Saudi Arabia, na kusababisha moto katika kituo kimoja wakati kituo kingine kikisitisha oparesheni zake kwa muda. 

Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia katika vita vya Yemen umesema mashambulizi hayo hayakusababisha majeruhi japo yalipiga moja ya sehemu muhimu za kampuni ya kuzalisha nishati, na kuharibu magari ya raia na nyumba. 

Muungano huo wa jeshi unaopigana nchini Yemen umesema ulifanikiwa kuharibu mashua inayoendeshwa kutokea mbali iliyokuwa imebeba vilipuzi kusini mwa bahari ya Sham. 

Mashambulizi hayo ya hivi karibuni yanaashiria ongezeko la mashambulizi ya waasi wa Kihouthi kwenye ardhi ya Saudi Arabia huku vita vya Yemen vikiingia mwaka wake wa nane na mazungumzo ya amani yakikwama.



from MPEKUZI

Comments