Serikali Itaendeleza Mazuri Yote Ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kuendeleza mazuri yote yaliyoachwa na Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na kuleta mema mengine mapya.

Rais Samia amesema hayo jana wakati wa maadhimisho ya kumbukizi ya mwaka mmoja ya kifo cha aliyekuwa Rais Hayati, Dkt. John Magufuli Wilayani Chato Mkoani Geita.  

Mhe. Rais Samia amemwelezea Hayati Magufuli kuwa Kiongozi aliyepinga rushwa na ubadhirifu, na kusisitiza uchapakazi na uzalendo kwa Taifa.  

Rais Samia amewaahidi wananchi wa Chato kuwa Serikali itakamilisha na kushiriki kuifungua miradi yote ya maendeleo ambayo imeshakamilika ikiwemo stendi mpya ya Chato, uwanja wa ndege wa Chato uliofikia asilimia 95 pamoja na kivuko cha Chato.

Vile vile, Rais Samia ametoa wito kwa wananchi wote kuendelea kuelimishana na kuhamasishana kushiriki katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi  litakayofanyika Agosti, 2022.

 



from MPEKUZI

Comments