Baada ya kutangaza kwamba Shirikisho la Urusi litatambua uhuru na kujitawala kwa mikoa inayounga mkono Urusi iliyojitangaza kujitawala mashariki mwa Ukraine, Vladimir Putin ameagiza jeshi la Urusi "kulinda amani" katika maeneo hayo, ambayo yaliyojitangaza kuwa jamhuri za watu wa Donetsk na Lugansk.
Sheria mbili za rais wa Urusi zinaomba Wizara ya Ulinzi kwamba vikosi vya jeshi vya Urusi vichukue "kazi za kulinda amani kwenye eneo" la jamhuri za watu za Donetsk na Lugansk. Hatua moja zaidi kuelekea kuongezeka kwa uhasama usiokoma. Rais wa Urusi wakati wa hotuba yake, alitambua maeneo yaliyojitenga, pia kauli yake ilikuwa ni ya vitisho na kujaribu kushambulia kwa baadhi ya mataifa.
Kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo, wanajeshi wa Urusi tayari wameanza kupelekwa katika maeneo hayo, magari ya kijeshi na magari ya kivita yanaelekea Donbass na baadhi tayari yapo kwenye mitaa ya Donetsk.
"Ukraine inaona vitendo vya hivi karibuni vya Urusi kama ukiukaji wa uhuru na uadilifu katika ardhi yetu", amejibu rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika hotuba kwa Taifa, akihakikisha kwamba Kiev haitaacha "sehemu ya nchi na haitaogopa " chochote au mtu yeyote".
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky pia alisema alitarajia uungwaji mkono "wa wazi" na "wenye ufanisi" kutoka kwa washirika wa Magharibi kwa nchi yake dhidi ya Urusi, baada ya utambuzi wa Moscow kwa "jamhuri" zilizojitangaza kutenga mashariki mwa Ukraine. "Ni muhimu sana kuona sasa rafiki yetu wa kweli ni nani," ameongeza.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment