Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akiwa kwenye runinga ya Fox News amesema mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine yaliyoanza Jumatano usiku wa kuamkia leo yasingefanyika wala kutokea wakati wa utawala wake.
Trump alipiga simu na kusema hakuamini kwamba Putin alitaka kufanya hivi mwanzoni.
"Nadhani alitaka kufanya jambo ili kufungua milango ya majadiliano, na hali ikawa mbaya zaidi, na ndipo akaona udhaifu," Trump alisema.
Zaidi ya hayo, Trump amesema kwamba anaamini uvamizi wa Urusi umechochewa kwa sehemu na "udhaifu" wa kujiondoa kwa Marekani kutoka Afghanistan.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment