TANZIA: Mwele Malecela Afariki Dunia


Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele katika Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk Mwele Malecela amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 58.

Dk Mwele amefariki dunia  Alhamisi Februari 10, 2022 jioni mjini Geneva, Uswisi wakati akipatiwa matibabu.

Kabala ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele wa WHO, Dk Mwele alikuwa Mkurugenzi wa Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika (Espen), wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika.

Dk Mwele ambaye ni mtoto wa Waziri Mkuu mstaafu, John Malecela, aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)



from MPEKUZI

Comments