Rais wa Marekani Joe Biden amejibu mashambulizi ya jeshi la Urusi yanayoendelea hivi sasa nchini Ukraine.
Anasema; "Sala za dunia nzima ziko pamoja na watu wa Ukraine". Rais Putin amechagua vita vya kutayarishwa ambavyo vitaleta maafa makubwa ya kupoteza maisha na mateso ya wanadamu
"Urusi pekee ndiyo inayohusika na vifo na uharibifu utakaoletwa na shambulio hili, na Marekani na washirika wake watajibu kwa umoja na njia madhubuti. Ulimwengu utaiwajibisha Urusi." anasema.
Biden anasema atahutubia Wamarekani leo siku ya Alhamisi kuhusu matokeo ambayo Urusi itakumbana nayo.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment