Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kuanza ujenzi wa majengo mapya katika kituo chake cha Umahiri cha Nishati Jadidifu Kilicho chini ya Chuo cha Ufundi Arusha kitakachokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 650 kwa wakati mmoja.
Akizungumza mara baada ya kukagua miundombinu iliyopo sasa katika kituo hicho Jijini Arusha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Carloyne Nombo amesema ujenzi huo umefadhiliwa na Mradi wa EASTRIP na unaolenga kuongeza fursa za mafunzo ya Mafundi wenye ujuzi na Stadi katika fani ya Umeme ambapo amesema miundombinu iliyopo ni ya zamani iliyojengwa na wajerumani miaka ya1930 na haitoshelezi pamoja na Chuo kwamba kiliendelea kutoa mafunzo.
Prof. Nombo amesema kituo hicho kupitia mradi pia kitawekekwa vifaa na mitambo mipya ya kisasa ya kufundishia na kujifunzia ili kiweze kutoa mafunzo yanayoendana na teknolojia ya kisasa na kuzalisha wataalam watakaoweza kushindani katika soko la ajira.
“Hiki kituo kilijengwa miaka 1930 na wajerumani kwa hiyo kina mitambo ya teknolojia ya kizamani kwa hiyo tunakijenga upya ili kiwe na uwezo wa kutoa mafunzo yanayoenda na ukuaji wa teknolojia, pia kiweze kusaidia katika kuzalisha wataalam watakaoshiriki katika kufanya kazi katika miradi ya kimkakati kama katika bwawa la Mwalimu Nyerere” amesema Prof. Nombo.
Katibu Mkuu huyo amesema Chuo kinapaswa kutambua kuwa kina deni la kuandaa wataalam hao kwa kuwa tayari miradi imeshaanza ikiwemo ule wa bwawa la Mwalimu Nyerere ambalo linawahitaji.
Naye Msanifu majengo wa kampuni ya Y & P Architects (T) limited Mringo Yassin aliyepewa jukumu la kubuni michoro ya miundombinu itakayojengwa katika kituo hicho ambapo amesema kazi hiyo itafanyika kwa miezi sita na ujenzi unatarajiwa kuchukua miezi 12 mpaka kukamilika.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment