Mwanaume Wa Miaka 30 Adaiwa Kumuoa Kwa Nguvu Binti Wa Miaka 14 Simanjiro.


Na John Walter-Manyara.
Jeshi la Polisi mkoani hapa linamshikilia Mwanaume mmoja mkazi wa kijiji cha Loswaki wilaya ya Simanjiro aliyejulikana kwa jina Lalahe Karoli (30) kwa tuhumza za kumtorosha na kwenda kuishi kinyumba na mtoto mwenye umri wa Miaka 14 kwa ridhaa ya Baba wa Mtoto.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Benjamin Kuzaga amethitisha tukio hilo ambapo amesema mbinu iliyotumika ni mtuhumiwa kumtorosha binti huyo na kumpeleka chumbani kwake na kumlazimisha kufanya nae ngono kisha kuishi nae kwa nguvu.

Kamanda Kuzaga amesema kwa kushirikiana na timu ya upelelezi na raia wema walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo kwa mahojiano zaidi.Pia Jeshi hilo limeeleza kuwa limemkamata Baba wa Mtoto aitwaye Lembris Salonic (60) mkazi wa Loswati Terati wilaya ya Simanjiro ndiye aliyeidhinisha kuolewa kwa binti yake huyo.

Kamanda Kuzaga ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi hilo kutoa taarifa ili kupambana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na watoto ambavyo vinarudisha nyuma Maendeleo ya mtoto na jamii kwa ujumla.


from MPEKUZI

Comments