Waziri wa Afya Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui Apata Uviko-19


Waziri wa Afya, Ustawi wa jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui amepata maambukizi ya ugonjwa wa Uviko-19 lakini hali anaendelea vizuri.

Akizungumza na Gazeti la Mwananchi, Mazrui amesema alibainika kuwa na ugonjwa huo juzi Desemba 24 baada ya kwenda kupimwa hospitalini.

“Siku ya Alhamisi nilianza kujisikia homa kali mafua, kuharisha nilienda hospitali kupima nikakutwa na maambukizi kwahiyo kwasasa nimejitenga nyumbani siendi kazini mpaka kipindi cha wiki moja niangalie hali itakavyokuwa,” amesema

Amesema hata mtu akienda kumtembelea nyumbani kwake kwa sasa wanaongelea dirishani ili kuepusha kusambaza maambukizi ya ugonjwa huo.

Amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zote dhidi ya ugonjwa huo na kuchanja akidai kwamba chanjo ndio imemsaidia kupunguza ukali wa ugonjwa huo

“Ugonjwa upo na watu wanaumwa lakini hawaendi hospitali kupimwa na kupata matibabu, wengi wanabaki nyumbani na kujitibu wenyewe, tutoke twende hospitalini, lakini wananchi waendelee kunawa mikono kuvaa barakoa na kuacha mikusanyiko isiyo ya lazima,” amesema

 

Credit:Mwananchi

 



from MPEKUZI

Comments