Waziri Simbachawene Akutana Na Maaskofu,manabii Na Mitume, Awataka Kulinda Amani Ya Nchi


WAZIRI wa Mambo ya Ndani George Simbachawene amekutana Maaskofu, Manabii na Mitume kutoka jumuiya ya makanisa ya Kipentekoste nchini  Desemba 18, 2021 katika kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa viongozi wa dini ndiyo wenye dhamana ya kuitunza amani ya nchi hii, amani kwenye taasisi za dini ndio amani ya nchi hii.

Amesema kuwa kama viongozi wa dini hawana maadili na hawakemei uovu kanisa hili litazaa watu wa aina gani?

Aidha Simbachewene amewakubalia mchakato wa kuanza kuwasajili mitume na Manabii wa Jumuiya ya makanisa ya Kipendekoste hapa nchini, pia ameshauri mchakato huo uwe wa uwazi, ili watakapotoka katika mkutano huo nchi ikawa katika Amani.

“Amani ya nchi yetu ndio kitu kikubwa kama hakuna  amani kwenye Familia, kama hakuna amani kwenye taasisi ya dini, kama hakuna amani kwenye dhehebu lako taifa linakuwa sehemu gani? Hii haiwezekani kukosa amani wakati tuna viongozi wa dini, mitume na Manabii.” Amesema Simbachawene.

Simbachawene amesema amani kwenye taasisi za dini ndio amani ya nchi, lakini kama viongozi wa dini sio waaminifu, au watuwake baadhi sio waadilifu na kanisa halikemei maovu taifa litazaa watu wa ajabu.

Amesema kuwa Viongozi wa dini wanategemewa katika kuimarisha amani ya nchi hii wakishirikiana na walinda amani wote.

Aidha wamewaasa jamii kutumia mitandao ya kijamii vizuri wakati huo huo wamesema kuwa changamoto kubwa ni kuwa na makanisa karibu na makazi ya watu pia wameiomba ruzuku kutoka serikalini kwaajili ya kuendeleza makanisa na huduma ya Mungu nchini.


from MPEKUZI

Comments