Watoto 119 Wenye TB Waokolewa


Na Lucas Raphael,Tabora

Serikali imewataka wadau wa Afya nchini kuangalia uwezekano na utaratibu wa Ufuatiliaji wa familia zenye wagonjwa wa kifua kikuu ili  uweza kuleta mafanikio makubwa  na kufanikiwa kuokoa Maisha ya Watoto zaidi ya 119 chini ya miaka mitano waliobainika kuwa na ugonjwa huo baada ya kufanyiwa uchunguzi katika mikoa ya Singida na Tabora.

Kauli hiyo ilitoklewa na mkurungezi wa  wa kinga kutoka  wizara ya Afya Dkt.Riziki Kisonga wakati wa kufunga shughuli za mradi wa CAP TB uliokuwa ukitekelezwa katika mikoa ya Tabora na Singida tangu mwaka 2017.

Alisema kwamba mradi huo umeweza kufanikisha kuibua wagonjwa wengi wa kifua kikuu chini ya miaka 5 jambo ambalo hapo awali lilikuwa linaondoa uhai wa watoto wengi bila kujulikana .

Dkt Kisonga alisema kwamba jitihada zinaendelea kufanywa na serikali katika kukabiliana na ugonjwa wa kifua kikuu uliokuwa chini ya mradi wa CAP TB unaoratibiwa na shirika lisilo la kiserikali la EGPAF.

Alisema kwamba mradi huo ulifanikiwa kuwafikia watoto 827,129 kwa uchunguzi  wa kifua kikuu kutoka 335 mwaka 2017 hadi 1852 mwaka huu .

Alisema kwamba kuongeza idadi ya watoto walioanzishiwa matibabu ya kifua kikuu kutoka 303 hadi 1851 kwa kipindi hicho kwa vituo vilivyofikiwa .

Awali  Mkurugenzi wa Ufundi Shirika la EGPAF Tanzania ,Dkt,Chirspin Kimario alimweleza mkurungezi wa kinga nchini kwamba  wanaishuru serikali ya awamu ya sita kwa jitiada nyingi walizoweka katika kufanikisha huduma za afya ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya ,kuweka mazingira wezeshi kwa wagonjwa wa kifua kikuu ili waweze kupata huduma bora za afya stahiki.

Hata hivyo walipongeza mpango wa taifa wa kifua kikuu na ukoma kwa kuwapa kipaumbele watoto katika mpango mkakati juu ya kifua kikuu

Alisema mradi huo ambao umetekelezwa katika halmashauri 12  za mikoa ya Tabora na Singida na kufikia vituo vya kutolea huduma za afya vipatavyo 45 ikiwemo 17 katika mkoa wa Tabora na 28 mkoani Singida  .



from MPEKUZI

Comments