Ufaransa: Watu 104,611 Wakutwa Na Covid-19 Ndani Ya Saa 24


Kwa mara ya kwanza nchini Ufaransa idadi ya watu 104,611 wameambukizwa virusi vya corona katika muda wasaa 24 zilizopita. Idadi hiyo haijawahi kufikiwa nchini humo tangu kuanza janga la corona.

Mamlaka ya afya ya Ufaransa imesema idadi ya wagonjwa wanaougua COVID-19 waliolazwa kwenye vitengo vya kuwahudumia watu wanaohitaji uangalizi mkubwa imepanda kwa wagonjwa 28 zaidi na kufikia jumla ya watu 3,282 waliolazwa kwenye vyumba hivyo vya watu mahututi.

Serikali ya Ufaransa itafanya mkutano kwa njia ya video leo Jumatatu ambapo Rais Emmanuel Macron pamoja na wakuu mabalimbali katika utawala wake watajadili hatua mpya za kujikinga na athari zinazosababishwa na janga la corona huku wasiwasi ukiwa unaoongezeka juu ya virusi vya aina ya Omicron vinavyoenea kwa haraka.


from MPEKUZI

Comments