Mahakama kutoa uamuzi mdogo kesi ya Lengai Ole Sabaya


Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha leo Jumatano Desemba 29, 2021 imepanga kutoa uamuzi mdogo kufuatia pingamizi lililowasilishwa na mawakili wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita.

Uamuzi huo mdogo unatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Patricia Kisinda anayesikiliza shauri hilo. Pingamizi hilo liliwasilishwa wakati shahidi wa 14 wa Jamhuri, Ofisa Uchunguzi kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Ramadhan Juma akiendelea kutoa ushahidi.

Desemba 17 mwaka huu, akiwasilisha hoja ya pingamizi hilo, Wakili wa utetezi Mosses Mahuna aliieleza Mahakama kuwa shahidi huyo hana uwezo wa kutambua watu kupitia ripoti hiyo ambayo hajaiandaa na wala siyo mtaalamu kutoka maabara za kiuchunguzi.

Alisema kuwa shahidi wa nane, Johnson Kisaka (Ofisa uchunguzi kutoka maabara ya kiuchunguzi ya Takukuru), aliieleza Mahakama kuwa hawezi kumtambua mtu kupitia ripoti hiyo.


from MPEKUZI

Comments