Mashirika Ya Kigeni Yazidi Kuvutiwa Kuwekeza Katika Sekta Ya Nishati Tanzania


 Na Dorina G. Makaya - Dar-es-Salaam.
Idadi ya mashirika ya kigeni yanayovutiwa kuwekeza katika sekta ya Nishati nchini yameendelea kuongezeka ikiwemo katika sekta ndogo ya umeme na nishati Jadidifu.

Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba, tarehe 29 Novemba, 2021, amekutana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mitsubishi iliyopo jijini Dar--es-Salaam, Kenji Nishizaki   na kujadili masuala ya ushirikiano wa kisekta na fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania.

Miongoni mwa masuala waliyoyazungumzia katika mkutano huo, uliofanyika kwenye ofisi ndogo za Wizara ya Nishati, ni pamoja na  kupanua wigo wa  biashara kwa kutazama fursa zilizopo za uwekezaji katika maeneo ya sekta ndogo  ya umeme, mafuta na gesi asilia pamoja na ushirikiano wa kisekta kwa ujumla na Serikali ya Tanzania

Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba, amewakaribisha Kampuni ya Mitsubishi kwa ajili ya kuwekeza hapa nchini na ameelekeza mashirika ya TPDC na TANESCO kutazama kwa upana zaidi wigo huo wa uwekezaji ambao Mitsubishi wanataka kuwekeza.


from MPEKUZI

Comments