Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Mhe Ummy Mwalimu amepiga marufuku wananchi kuachangishwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa yanayojengwa na fedha zilizotolewa kwa ajili ya UVIKO 19
Ametoa agizo hilo jana wakati akikagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mkoani Iringa
Ameendelea kufafanua kuwa Serikali haikatazi wananchi kuchangia nguvu kazi kwa kuwa wamekuwa wakijitoa katika kutekeleza miradi ya maendeleo ili kuunga mkono juhudi za Seikali katika kuleta maendeleo
Amesema kuwa ujenzi wa Madarasa kwa fedha za UVICO 19 zimeletwa za kutosha na zinajitosheleza hadi kukamilika kwa ujenzi huo hivyo wananchi wasilazimishwe kuchangia fedha za ujenzi huo
Waziri Ummy amesema kuwa anashangazwa na maelezo ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ya kuwatoza wananchi shilingi 5000 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Madarasa hayo
"Fedha zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa l ya kidato cha kwanza zinajitosheleza hadi ukamilishaji wake, inanishangaza ninyi mnawataka wananchi wachangie, naagiza ni Marufuku kwa wananchi kuchangishwa fedha kwa ajili ya ujenzi ' Waziri Ummy
Ameendelea kusema kuwa wananchi wanatakiwa kuchangia nguvukazi kwa kusaidia kuchimba msingi, kubeba mawe, kuchota maji, kusogeza mchanga na kubeba matofali, na sio kutozwa fedha
Aidha, uchangiaji wa mwananchi si lazima bali ni ihari na pia wananchi kwa hiari yao wanaweza kuchangia vifaa vya ujenzi kadri watakavyoona inafaa lakini sio kulazimishwa kuchangishwa pesa.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment