Mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa michezo ‘CAS’ imetupilia mbali Rufaa ya klabu ya Yanga, dhidi ya mchezaji Bernad Morrison Raia wa Ghana na kumfanya mchezaji huyo kuwa halali kuitumikia klabu ya Simba.
Uamuzi wa mahakama hiyo, umetolewa tarehe 21, Novemba 2021, mwaka huu katika taarifa yao kwa vyombo vya habari mara baada ya kusikiliza shauri 29 Julai, mwaka huu kwa pande zote mbili kwa njia ya video kwa kuwasilisha vielelezo vya ushahidi.
Shauri hilo lilianza kusikilizwa mara baada ya CAS kuondoa pingamizi la awali (Preliminary Objection) lililowekwa na Bernard Morrison kwa kutaka kesi hiyo kusikilizwa nchini.
Kufuatia kuondolewa kwa pingamizi hilo Juni 2 mwaka huu, Mahakama hiyo ilitaka pande zote mbili kutuma mapendekezo ya namna gani kesi itasikilizwa, kwa kutumia njia ya nyaraka au maneno (mtandao).
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment