Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), limemtaja mwanafunzi aliyehitimu shule ya msingi St Anne Marie iliyopo mkoani Dar es Salaam, Eluleki Evaristo Haule kuwa ndiye aliyeibuka kinara katika matokeo ya mtihani ya Darasa la Saba 2021.
Akitangaza matokeo hayo leo Jumamosi Oktoba 30, 2021 Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema watahiniwa bora kitaifa ni wale ambao wamepata alama nyingi zaidi kuliko wenzao kwenye masomo sita waliyotahiniwa.
Alimtaja aliyeshika nafasi ya pili kuwa ni Happy Joseph Deus kutoka shule ya msingi Twibhoki ya Mkoa wa Mara na nafasi ya tatu ikienda kwa John Chacha Charles kutoka Twibhoki.
Aliyeshika nafasi ya nne ni Joshua Mahende Jacob kutoka shule ya msingi Twibhoki iliyopo Mara pia, Eva Sebastian Chengula kutoka shule ya msingi Fountain of Joy ya Dar es Salaam ameshika nafasi ya tano, Joctan Samwel Matara kutoka Twibhoki ameshika nafasi ya sita.
Barnaba Jumanne Magoto kutoka shule ya msingi Twibhoki ipo Mara ameshika nafasi ya saba, Rahma Ombi Juma kutoka shule ya Mtuki Highland iliyopo Dar es Salaam ameshika nafasi ya nane na nafasi ya tisa ni Juliana John Shimbala kutoka St Joseph’s nafasi ya kumi ameishika Jackline Manfredy kutoka shule ya Masaka iliyopo Dar es Salaam.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment