Jeshi la Polisi linawatangazia vijana wote waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi Nchini kuwa wanatakiwa kuripoti Shule ya Polisi Moshi kuanzia tarehe 23/10/2021 hadi tarehe 29/10/2021.
Kwa vijana waliofanyiwa usaili Baracks Dar es Salaam kwenye vikosi ambavyo vipo chini ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi watatakiwa kuripoti Makao Makuu ya Polisi Dodoma 24/10/2021 saa 2.00 asubuhi wakiwa na nauli zao kwa ajili ya safari ya kwenda Shule ya Polisi Moshi.
Kwa waliofanyiwa usaili Mikoani wanatakiwa kuripoti kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa waliofanyia usaili tarehe 22/10/2021 saa 2.00 asubuhi kwa ajili ya kupewa utaratibu wa safari ya kwenda Shule ya Polisi Moshi.
Pamoja na maelekezo yaliyotolewa kwenye tangazo la tarehe 19/10/2021 kila mmoja atatakiwa kuja na Tsh 40,000 kwa ajili kupima afya.
Kijana yeyote atakaye ripoti Shule ya Polisi Moshi baada ya tarehe 29/10/2021 hatopokelewa na atahesabika amejiondoa mwenyewe kwenye mafunzo.
👉Kuona majina ya waliochaguliwa kujiunga na jeshi la Polisi,BOFYA HAPA.
👉Kupata nafasi mbalimbali za kazi serikalini na makampuni binafsi,BOFYA HAPA
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment