Kumbukumbu za Simu ya Ole Sabaya Zapokelewa Mahakamani


Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imetupilia mbali pingamizi la kutaka nyaraka mbalimbali zikiwemo kumbukumbu za kupiga na kupokea simu, kutuma na kupokea ujumbe mfupi wa simu za aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake, zisipokelewe kama kielelezo katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili.

“Mahakama imeona pingamizi halina msingi kwa sababu imereja ushahidi aliotoa shahidi kuhusiana na hati hiyo iliyopingwa na kuona shahidi alieleza mahakama aliandaa hati hiyo kwa ajili ya kuonyesha uhalali wa kazi aliyofanya.

“Hivyo basi mahakama baada ya kuangalia hati hiyo imeona ime-cover (imegusia) vyote alivyoelezea shahidi na kwa sababu hiyo imetupilia mbali pingamizi hilo kwa kutokuwa na mashiko na kuvipokea vielelezo vyote kwa pamoja kama kielelezo cha tatu,”

Pingamizi hilo lililetwa na wakili wa utetezi Edmund Ngemela wakati Meneja wa Ulinzi wa kampuni ya simu za mkononi Vodacom James Wawenje alipokuwa akiendelea kutoa ushahidi wake mahakamani leo.


from MPEKUZI

Comments