Na. John Mapepele, WUSM
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Innocent Bashungwa ameomba mashindano ya Kombe la Taifa, (Taifa CUP) yaliyorejeshwa na Wizara yake mwaka huu kuitwa Kombe la Taifa la Mama Samia (Samia Taifa CUP) kutokana na uzito wa mashindano hayo na nia njema ya Mhe, Rais ya kuendelea michezo nchini.
Mhe. Bashungwa ameyasema hayo Oktoba 27, 2021 kwenye hafla ya kupongeza timu ya soka ya Taifa ya Wanawake (Taifa Stars) iliyoandaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan jijini Dar es Salaam alipokuwa akifafanua mafanikio ya Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo katika kipindi hiki.
Akielezea mafanikio hayo amesema kuwa ni pamoja na kuandaa mkakati pamoja baina ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Baraza la Michezo la Majeshi Tanzania (BAMMATA) na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwenye mashindano ya kimataifa na kuongeza kuwa wachezaji 46 wanacheza michezo ya kulipwa nje ya nchi.
Kuhusu maelekezo ya Mhe. Rais ya kuwa na shule za michezo nchini, Mhe. Bashungwa amesema hadi sasa zimeshatengwa shule za michezo 56 ambapo ni mbili kila Mkoa ambazo zitakuwa zinatoa masomo maalum ya michezo na kwamba shule hizo zitapatiwa vifaa na walimu kwa ajili ya michezo.
Amesema tayari shilingi bilioni 1.6 zimetengwa kwa ajili ya chuo cha michezo (National Sports Academy) cha Malya mkoani Mwanza pia michoro kwa ajili ya kumbi za kisasa za michezo (sports Arena) zinatarajiwa kukamilika mwezi ujao.
Aidha, amesema Wizara imeandaa mpango mkakati ambao umeainisha michezo michache (6) ya kipaumbele ili iweze kufanya vizuri na kufika kwenye ngazi ya kimataifa.
Pia, katika kuendeleza michezo kwa wanawake Tamasha la michezo la Wanawake la Tanzanite lilifanyika Septemba 16-18, 2021 jijini Dar es Saaam ambapo litaendelea kuboreshwa na kuwepo kila mwaka ili kuibua vipaji vya wanawake.
Amesema hadi sasa tayari Wizara imekamilisha marekebisho ya uwanja wa Taifa wa ndani ambao umetoa fursa ya kufanyika kwa mashindano ya Kanda ya Afrika ya Kikapu kwa wanaume na wanawake yanayoanza Oktoba 29,2021 ambapo zaidi ya nchi kumi zinashiriki.
Pia maboresho ya uwanja wa Mkapa na uhuru yamekamilika yanayotoa fursa ya kufanyika kwa mashindano ya Afrika ya Soka kwa walemavu Novemba mwaka huu, na kuongeza kuwa michezo ya SHIMIWI imerejeshwa ambayo ilifunguliwa Oktoba 23,2021 na Makamu wa Rais.
Bashungwa amefafanua kuwa endapo Wizara itawezeshwa zaidi, na mikakati iliyojiwekea pamoja na maelekezo yanayotolewa na viongozi wakuu michezo, Sanaa na utamaduni utafiuka mbali.
Akitambulisha wageni wa Wizara kwenye tukio hilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amemshukuru Mhe. Rais kwa kuleta mapinduzi makubwa kwenye Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo na kumwahidi kuendelelea kusimami kikamilifu ili kuendeleza michezo.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment