393 wafutiwa matokeo ya mtihani, NECTA yaagiza wahusika wachukuliwe hatua


Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), limefuta matokeo yote ya watahiniwa 393 waliobainika kufanya udanganyifu katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kwa mwaka 2021.
 

Taarifa hiyo imetolewa leo Oktoba 30, 2021, na Katibu Mtendaji wa baraza hilo Dkt. Charles Msonde, na kusema kwamba NECTA imezishauri mamlaka zinazohusika, kuwachukulia hatua kwa mujibu wa kanuni za utumishi na sheria za nchi wale wote waliohusika ama kusababisha kutokea kwa udanganyifu huo.

Aidha Dkt. Msonde akizungumzia ufaulu amesema kwamba, idadi ya watahiniwa waliofaulu kwa mwaka 2021 imeongezeka kwa watahiniwa 74, 130 sawa na asilimia 8.89 ikilinganishwa na mwaka 2020, ambapo somo la Kiswahili limeongoza kwa wanafunzi kufaulu huku ufaulu katika somo la English ukishuka na kuwa na asilimia 48.02.

 

 



from MPEKUZI

Comments