Naibu Waziri wa Ardhi Dkt. Mabula Asitisha Makampuni 3 Ya Upimaji Wilaya Ya Bahi Dodoma


Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabula amesitisha makampuni matatu yaliyokuwa yakifanya urasimishaji makazi katika wilaya ya Bahi mkoani Dodoma kwa kushindwa kukamilisha kazi kwa wakati.

Naibu Waziri wa Ardhi alisema hayo wilayani Bahi mkoani Dodoma wakati akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya wilaya hiyo akiwa katika muendelezo wa ziara yake katika wilaya za mkoa wa Dodoma.

Aidha, ameagiza ofisi ya ardhi mkoa kukaa na mkurugenzi wa halmashauri ya Bahi iundwe na timu ya mkoa ije hapa kwa gharama ya mkurugenzi ili kukamilisha upimaji.

Naye Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Dodoma Thadei Kabonge amesema Kumeibuka tabia kwa wakazi wa maeneo mbalimbali kutojitokeza kuchukua hati zao za umiliki wa ardhi kwa wakati kwa kigezo cha kukwepa kulipa kodi ya pango ardhi kitu ambacho kwa sasa Bunge limeipatia muarubaini tabia hii.

Kabonge ameongeza kuwa mwaka jana Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha sharia kwamba ardhi ikishapimwa na ikapita miezi mitatu na mmiliki hajajitokeza kuja kumilikishwa basi itahesabika tayari ushamilikishwa na itaanza kuhesabiwa kodi ya ardhi.

Aidha, Kabonge wametakiwa wananchi kujitokeza ili kumilikishwa Ardhi kisheria kwa kukwa kutomilikishwa ardhi sio kigezo cha kukwepa kulipa kodi ya ardhi hata kama ardhi hiyo itakuja kumikishwa baada ya miaka kupita.

Kamishna Kabonge amebainisha kuwa ofisi yake ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Dodoma ina viwanja zaidi ya 2,550 ambavyo vimepimwa tayari lakini wananchi hawataki kumilikishwa.


from MPEKUZI

Comments