Korea Kaskazini yarusha kombora la Hypersonic


Korea Kaskazini imefanikiwa kurusha kombora la Hypersonic linaloitwa Hwasong-8, siku ya Jumanne  Septemba 28, shirika la habari la serikali, KCNA, limesema leo Jumatano.

Makombora ya Hypersonic yana kasi zaidi na wepesi zaidi kuliko yale ya kawaida, na kuifanya iwe ngumu sana kwa mifumo ya ulinzi wa makombora kuyazuia, kulingana na shirika la habari la AFP.

Kufanikiwa kwa jaribio hili ni "kwa umuhimu mkubwa wa kimkakati" kwani Pyongyang inataka "kuzidisha mara elfu" uwezo wake wa ulinzi, KCNA imesema.

Kombora hilo jipya lilikuwa moja wapo ya mifumo "mitano muhimu zaidi" ya silaha iliyowekwa katika mpango wake wa maendeleo ya kijeshi wa miaka mitano, vyombo vya habari vya serikali vimebaini.


from MPEKUZI

Comments