Majina ya Waliochaguliwa na NACTE Kujiunga Vyuo mbalimbali Program za Afya na Sayansi Shirikishi 2021/2022
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa elimu ya ufundi na mafunzo katika Vyuo ambavyo si Vyuo Vikuu ama Vyuo Vikuu Vishiriki nchini.
Jukumu mojawapo la Baraza ni kuhakikisha kuwa mafunzo yanayotolewa katika Vyuo vya Ufundi nchini yanakidhi vigezo na ubora unaohitajika katika soko la ajira ndani na nje ya nchi.
Pia Baraza linao wajibu wa kuratibu udahili wa Wanafunzi kwenye Vyuo na kozi/programu zinazotambulika na mamlaka husika.
Baraza liliratibu udahili wa waombaji wa mafunzo ya Afya na Sayansi Shirikishi Ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa mwaka wa masomo 2021/2022 kwa Vyuo vya Afya vinavyomilikiwa na Serikali. Dirisha la udahili lilifunguliwa tarehe 27 Mei, 2021 na kufungwa tarehe 13 Agosti, 2021.
Baraza linapenda kuufahamisha umma kwamba udahili wa wanafunzi wa programu za Afya katika Vyuo vya Serikali umekamilika.
Jumla ya maombi 21,939 yalipokelewa kupitia mfumo wa udahili (Students Admission Verification). Kati ya hao, waombaji 17,664 walikuwa na sifa za kuchaguliwa katika nafasi mbalimbali za masomo katika Vyuo vya Afya. Waombaji waliochaguliwa ni 3,478 ikiwa ni sawa na 19.69% ya waombaji wote wenye sifa.
Hata hivyo, jumla ya waombaji 14,186 wenye sifa hawakuchaguliwa kutokana na ufinyu wa nafasi katika Vyuo vya Afya vya Serikali. Waombaji waliotuma maombi wanaweza kuangalia majibu yao kupitia tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz) kwa kubofya “Selection Results 2021/2022.
Hivyo, Baraza linawashauri waombaji wenye sifa waliokosa nafasi za masomo katika vyuo vya Afya vya Serikali kuomba katika vyuo vya Afya vya Binafsi.
==>>Kuona Majina ya Waliochaguliwa,BOFYA HAPA
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment