Makamu Wa Rais Amsimamisha Kazi Mkurugenzi Nanyumbu


 Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango, jana Julai 24, 2021 amefanya ziara ya kustukiza katika stendi ya Mabasi ya Mangaka iliopo Wilaya ya Nanyumbu.

Makamu wa Rais amekasirishwa na uongozi wa Wilaya kufanya upotevu mkubwa wa fedha  usiolingana na matokeo ya ujenzi wa mradi huo.Ujenzi wa majengo ya stendi hiyo umetumia shilingi bilioni 2.2 kiasi ambacho Makamu wa Rais amesema hakilingani na ujenzi huo.

Makamu wa Rais amemuagiza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Dkt. Festo Dugange kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu Hamis Dambaya ili kupisha uchunguzi kutoka vyombo husika.

Amesema viongozi hawana budi kusimamia fedha za serikali zinazopelekwa katika maeneo yao ili kuwaletea maendeleo wananchi.



from MPEKUZI

Comments