Na Lucas Raphael Tabora
Katika hali isiyokuwa ya kawaida fisi aliingia ndani ya nyumba na kumnyakua mtoto wa mwaka mmoja na kisha kukimbia naye na kumjeruhi vibaya kisha kumsabishia kifo huku akiwajeruhi watu watatu na mmoja amelezwa katika hospital ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Tabora kamishna Msadizi Safia Jongo Akizungumzia tukio hilo alisema lilitokea julai 25 mwaka huu majra ya saa 9 usiku katika kijiji cha kangeme kata ya Zungimlole wilaya ya Kaliua Mkoa Tabora
Alisema kwamba Tukio hilo limetokea katika hifadhi ya Luganzo Tongwe Kijiji cha Kangeme kata ya Zugimlole wilaya ya kaliua mkoani hapa ambapo fisi huyo alitoka hifadhini na kuingia ndani ya nyumba ya Nhganya Mayala (45) muda wa majira ya saa 9 usiku na kumchukua Mtoto na kumjeruhi vibaya jambo lililosababisha kifo chake.
Alisema kwamba watu watatu akiwemo baba mzazi wa mtoto hiyo walijeruhiwa walipojaribu kumshambulia fisi huyo.
“Baadhi ya wananchi waliposikia lile tukio na katika hali ya kupambana na yule fisi aliweza kuwajeruhi watu watatu na wamejeruhiwa vibaya na mmoja yupo hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora kitete kutokana na hali yake kuwa mbaya zaidi”alisema
Aliongeza kuwa baadae askari polisi wakishirikiana na maafisa wanyamapori walienda kukagua tukio na kuona hali ikoje fisi huyo tena aliibuka na kuanza kuwashambulia askari na watu waliokuwa wakitoa taarifa kwa askari
“Askari walipambana na kufanikisha kumuua huyo fisi lakini katika mapambano hayo risasi 49 zimepotea kwa kumpiga tu ”aliongeza kamanda jongo
Kwa upande wao baadhi wa wananchi wa kijiji cha Kangeme kata ya Zugimlole walisema kuna idadi kubwa ya fisi katika eneo la hifadhi hiyo .
Waliendelea kusema kwamba wameingiwa na hofu kutoka na hali ya hatari kuanza kujitokeza na kuwaomba maafisa wanyamapori kufanya dolia za mara kwa mara kuzungukia katika hifadhi hiyo.
Kamishna msaidizi wa jeshi la polisi safia jongo aliwataja watu waliojeruhiwa ni baba wa mtoto huyo ni Nganya Mayala 45 ambaye kang’atwa kingaja cha mkono wa kulia,Ngezi Lega 25 kang’atwa mkono wa kushoto na paja na Tule Malongo miaka 45 aliyevunjwa taya na kung’atwa mkono wa kushoto ambaye amelazwa katika hospitali Rufaa ya mkoa wa Tabora kitete.
mwisho
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment