Dr. Gwajima: Fanyeni Ajenda Ya Upatikaji Wa Dawa Iwe Ya Kudumu


 Na.WAMJW- Dodoma.
Wafamasia nchini wametakiwa kufanya ajenda ya upatikanaji wa dawa iwe ya kudumu Kwenye kamati za ulinzi na usalama ngazi ya Kijiji, Kata,Wilaya na Mkoa.


Rai hiyo imetolewa jana na Dkt.Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati wa mafunzo ya usimamizi na UDHIBITI wa bidhaa za afya kwa wafamasia wa Mikoa,Halmashauri na Hospitali uliofanyika jijini Dodoma.


Dkt. Gwajima amesema kuwa ajenda hiyo ikiwa endelevu Kwenye ngazi hizo Basi hakutakuwa na malalamiko ya upatikanaji wa dawa yanayoendelea kuwa hauridhishi 


“Nitoe maagizo kwa viongozi wa ngazi zote ,wafamasia wa Mikoa,Halmashauri na Hospitali fanyeni ajenda ya upatikanaji wa dawa iwe ya kidumu Kwenye kamati za ulinzi na usalama ngazi ya Kijiji, Kata, Wilaya na Mkoa”.Alisisitiza.


Hata hivyo Dkt.Gwajima aliwataka wafamasia hao kuimarisha kamati za Dawa na Tiba Katika ngazi zote “Mfamasia  ndiye Katibu wa kamati za Dawa na Tiba lakini kamati hizi hazifanyi kazi zimekufa,naelekeza kuwa wote ambao kamati zao zilibainika kuwa mfu watoe maelezo kwa mamlaka zao za ajira na kwa Baraza lao la kitaaluma.


Aidha, Waziri huyo aliwaagiza wataalamu hao kwenda kusimamia Mwongozo wa Matibabu nchini na Orodha ya Taifa ya Dawa Muhimu (STG/NEMLIT),kwani mwongozo huo toleo  jipya la mwaka 2021  limezinduliwa.


“Andikeni dawa kwa kuzingatia  mwongozo huu na kuwe na mfumo wa tathmini kwa wale wasiotii kuandika majina halisi ya dawa (generic names) Bali wanaandika majina ya Biashara zao(brand names) mkasimamie mwongozo huu”Alisema.


Kwa upande wa matumizi ya Cheti Cha Dawa Dkt. Gwajima aliwataka wafamasia hao Kwenye kusimamia Hilo Kama alivyoelekeza awali kanuni ya Cheti Cha dawa ‘The Pharmacy (Prescription Handling and Control Regulations, 2020) kwani imeandaliwa na imeanza kutumika.


“Sekta ya afya na hasa waandishi na watoaji wa dawa fuatieni kanuni hii kinyume na hapo utashtakiwa  tu maana haitajulikana Nani alikunywa dawa”.


Dkt.Gwajima aliwataka wafamasia hao kuhakikisha Kuna upatikanaji na matumizi sahihi ya nyezo muhimu za usimamizi wa bidhaa za afya zikiwemo leja ya Mali na hati yabkutoa na kupokea Mali,rejista ya dawa,rejista ya sindano na Cheti Cha dawa.



from MPEKUZI

Comments