SERIKALI za Tanzania na Poland zimeingia makubaliano ya kuimarisha huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kwenye majiji ya Dodoma na Dar es Salaam kupitia utekelezaji wa ujenzi wa miradi wa majitaka katika Mji wa Serikali , kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji kwa Jiji la Dodoma na kupunguza kiwango cha upotevu wa maji kwa Jiji la Dar es Salaam .
Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi ( Mb ) amesema makubaliano ya Tanzania na Poland ni hatua muhimu kwa Serikali katika kufikia malengo ya kuimarisha huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kwenye makao makuu ya nchi Dodoma ambayo kutokana na kasi ya maendeleo na ongezeko la watu kumesababisha mahitaji makubwa ya maji kwa jiji hilo .
Mhandisi Mahundi amesema Serikali imejizatiti kumaliza tatizo la upotevu wa maji katika Jiji la Dar es Salaam ambalo kimsingi ni jiji la biashara ni muhimu maji yanayozalishwa yafike kwa kiwango cha kutosha ili kuchochea shughuli za maendeleo na kuongeza mapato kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam ( DAWASA ) yatakayotumika kufanikisha utekelezaji wa mipango yake .
Aidha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje , anayesimamia ushirikiano wa Kiuchumi na aendeleo Bara la Afrika na Mashariki ya Kati , Mhe . Pawel Jablonski amesema kuwa Poland ipo tayari kutekeleza makubaliano yaliyoafikiwa kwa lengo la kuendeleza Sekta ya Maji Tanzania na kuimarisha ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili .
Ujumbe kutoka nchini Poland uliongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje , anayesimamia Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo Bara la Afrika na Mashariki ya Kati , Mhe . Pawel Jablonski , Balozi wa Poland nchini Tanzania , Mhe . Krzysztof Buzalski pamoja na maafisa waandamizi kutoka Serikali ya Poland .
Makubaliano hayo ni matokeo ya majadiliano ya takribani miaka mitatu tangu Serikali hizo zilipokutana kwa lengo la kukuza na kuimarisha ushirikiano kwenye Sekta ya Maji nchini .
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment