RC Makalla Awataka Wananchi Kuchukuwa Tahadhari Dhidi Ya Corona.


 Kufuatia kuwepo kwa Viashiria vya Mlipuko wa Ugonjwa wa Corona, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amewataka Wananchi kuchukuwa tahadhari na kuziagiza Taasisi na sehemu zote za mikusanyiko kuweka ndoo za Maji na Miundombinu ya Maji tiririka.


Akitoa tamko la tahadhari dhiri ya Corona RC Makalla amesema Kutokana na Mwingiliano wa watu kutoka Nchi jirani na Nchi mbalimbali na Mikoa mingine wameona ni vyema kutoa tahadhari kwa Wananchi.


Miongoni mwa tahadhari ambazo RC Makalla amewataka Wananchi kuzichukuwa ni pamoja na :-


1.Kuvaa kwa Usahihi Barakoa kila wawapo sehemu za mikusanyiko, vyombo vya usafiri, Masoko, sherehe, maofisini na vituo vya Afya.


2. Kunawa Mikono kwa Maji tiririka kwa sabuni Mara kwa Mara.


3.Wananchi kuwahi mapema vituo vya Afya wanapobaini dalili za Corona ikiwemo homa Kali, mafua Makali, kikohozi, uchovu na nyingine.


4. Kufanya Mazoezi ili kuimarisha Kinga ya Mwili.
5. Kula mlo kamili.
6. Uangalizi mzuri kwa watu walio kwenye hatari ya kupata madhara* wakiwemo Wazee na Wenye Magonjwa sugu.


Aidha RC Makalla amewaelekeza Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Taasisi za Umma na za kiraia na Vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanasimamia ipasavyo maelekezo hayo.



from MPEKUZI

Comments