Kada wa CHADEMA Mdude Nyagali Aaachiwa Huru

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya imemuachia huru kada wa Chadema, Mdude Nyagali aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kukutwa na dawa za kulevya baada ya mahakama kueleza kuwa ushahidi uliotolewa dhidi yake ni batili.
 
Juni 14, 2021, Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya iliahirisha kutoa hukumu dhidi ya kesi yake kwa kile kilichoelezwa kuwa hukumu bado haijakamilika pamoja na mambo mengine ambayo yalikuwa nje ya uwezo wa Hakimu.


from MPEKUZI

Comments