Jacob Zuma. Ahukumiwa Miezi 15 Jela


Mahakama nchini Afrika Kusini imemhukumu kifungo cha miezi 15 aliyekuwa rais wa taifa hilo, Jacob Zuma.

Hii ni baada ya Korti ya Katiba kumpata na hatia ya kukaidi agizo la kufika mahakamani baada yakukosa kufika kwenye kikao cha uchunguzi wa kesi ya ufisadi wakati alipokuwa rais.

Mahakama ilikuwa na jukumu la kuamua kama Bw.Zuma anapaswa kuadhibiwa kwa kukataa wito wa mahakama na amri ya mahakama ya kumtaka afike mahakamani kutoa ushahidi kuhusu shutuma za rushwa wakati wa utawala wake.

Mwenyekiti wa kamati maalum ya uchunguzi wa mahakama ,Raymond Zondo ambayo imekuwa ikichunguza madai hayo aliiomba mahakama itamke kuwa rais huyo wa zamani alidharau mahakama na imhukumu kifungo cha miaka miwili.

Tangu alipojiuzulu mnamo mwaka 2018,  Zuma amekuwa akifika mahakamani akikabiliwa na shutuma za ufisadi ambazo amekuwa akizikanusha.


from MPEKUZI

Comments