Bunge lapata wawakilishi 20 wa mabunge mengine Duniani


Wabunge Ishirini wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamechaguliwa kuliwakilisha bunge hilo katika mabunge mengine duniani, na wengine sita wamechaguliwa kuingia katika Tume ya Huduma za Bunge.

Wabunge hao wamechaguliwa baada ya majina yao kupitishwa kwenye Kamati za vyama vyao, lakini hawakupigiwa kura kutokana na idadi yao kulingana na nafasi zilizokuwa zikitakiwa.

Spika wa Bunge Job Ndugai ameliambia Bunge jijini Dodoma kuwa uchaguzi huo umefanyika kutokana na kuanza kwa bunge jipya la 12, baada ya waliokuwa Wawakilishi kumaliza muda wao.

Waliochaguliwa kwa kura ya ndio katika Bunge la dunia (APU) ni Esther Matiko, Mwanaisha Ulenge, Ramadhan Suleiman Ramadhan, Joseph Mhagama na Elibarick Kingu.

Kwa upande wa Bunge la Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) waliochaguliwa ni Shari Raymond, Kassim Hassan Haji, Seleman Zedi, Dkt. Afred Kimea na Hawa Mwaifunga.

Spika Ndugai amewataja Wabunge waliochaguliwa kuingia katika Bunge la Afrika kuwa ni Ngh’wasu Kamani, Turfik Salim Turik, Jerry Silaa, Nape Nnauye na Anatropia Theonest.

Waliochaguliwa kwenda Bunge la Umoja wa nchi za Maziwa Makuu ni Dkt. Christina Ishengoma, Najma Giga, Ezra Chiwelesa, Deus Sangu na Shamsia Mtamba.

Kwa mujibu wa taarifa ya Spika Ndugai Bungeni, Wabunge waliochaguliwa kuingia katika Tume ya Huduma za Bunge ni Aesh Hillary, Rashid Shangazi, Halima Mdee, Fakharia Shomari, Janejelly Ntate, Zahoro Mohamed na Khalifa Mohamed Issa.



from MPEKUZI

Comments