Zuma akanusha mashtaka ya ufisadi dhidi yake


Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma amekana mashtaka yote 18 ya ufisadi anayokabiliwa nayo katika mahakama ya Pietermaritzburg nchini humo.

Jacob Zuma alisema anapinga makosa yote 18 ya ulaghai, ufisadi, ulaghai, ukwepaji wa kodi na utakatishaji fedha haramu.

Mashtaka hayo yanahusiana na matukio ya zaidi ya miongo miwili - katika siku za mwanzo za demokrasia ya Afrika Kusini - pamoja na mpango mkubwa wa silaha ..

Zuma na washirika wake wanasisitiza kuwa kesi hiyo ni ya kisiasa.Umati wa watu umekusanyika nje ya ukumbi wa mahakama huko Pietermaritzburg kuashiria kuwa Zuma bado ana umaarufu miongoni mwa wafuasi wake.



from MPEKUZI

Comments