Serikali imewaagiza wamiliki wa viwanda vya chuma nchini kukaa kikao cha pamoja kwa ajili ya kujadili na kukubaliana kuhusu teknolojia sahihi ya kuchambua vyuma chakavu ambayo itakuwa na uwezo wa kutambua vitu vyenye milipuko wakati wa kufanya uchakataji wa vyuma hivyo ili kutengeneza bidhaa mbali mbali za chuma.
Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Patrobas Katambi, alipofanya ziara katika viwanda vya Fujian Hexingwang na Lodhia Group of Companies vilivyopo Mkuranga kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya kuboresha mazingira ya kazi yaliyotolewa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) hivi karibuni.
“Wote wanaofanya bishara zinazohusiana na kuchakata chuma wakae katika kikao cha pamoja watafute teknolojia itakayo tusuaidia kugundua malighafi zenye mlipuko ili kuepuka ajali zinasababishwa na uchambuzi usiofaa wa malighafi ya viwanda hivyo hali ambavyo inasababisha kutokea ajali nyingi ambazo baadhi yake zimekuwa zikigharimu uhai wa Watanzania wenzetu,” amesema Naibu Waziri Katabi.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, ambaye aliambatana na Naibu Waziri katika ziara hiyo amesema lengo la ziara hiyo ni kufuatilia maagizo ambayo yalitolewa na OSHA hivi karibuni wakati Taasisi yake ilipokuwa ikichunguza ajali iliyotokea katika kiwanda cha Fujian Hexingwang ambapo ajali hiyo ilisababisha vifo vya wafanyakazi wawili.
Ameleza kuwa pamoja na wamiliki wa kiwanda hicho kupewa maelekezo juu kuboresha mazingira ya ufanyaji kazi baada ya tukio la ajali kutokea na kugharimu maisha ya wafanyakazi lakini bado kiwanda hicho hakijatekeleza kwa kiwango kikubwa.
“Tumekuja kuangalia utelezaji wa maagizo tuliyoyatoa ili tufungue kiwanda hiki kiendelee na shughuli zake lakini bado hawajatekeleza na sababu ya kutotekeleza tumebaini ni kutokana na wenye kiwanda hiki kuwa na uelewa mdogo kuhusiana na mambo tuliyowaelekeza. Hivyo, japokuwa kazi ya kutengeneza mifumo ya Usalama na Afya mahali pa kazi ni wajibu wao lakini tumeamua kwamba tutaleta watalaam wetu ili waweze kuwaongoza kwa karibu kusudi wakamilishe marekebisho hayo muhimu na kisha tuwaruhusu kuendelea na uzalishaji,” ameeleza Kiongozi huyo Mkuu wa OSHA.
Aidha, amesema Taasisi yake kwasasa inafanya ukaguzi wake kisekta kwa kuzingatia hali ya vihatarishi vya kiusalama na afya (risk-based inspections) ambapo wamekwisha fanya katika sekta kadhaa ikiwemo madini, fedha na hifadhi kwa jamii.
“Kwasasa tunaendelea na ukaguzi katika viwanda vya chuma kote nchini. Baada ya kukamilisha ukaguzi huu na kuandaa repoti tutazishirikisha mamlaki nyingine zikiwemo Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja ya Uwekezaji ili wanapoandaa sera, sheria na miongozo mbali mbali ya uwekezaji wahakikishe kwamba miongoni mwa matakwa muhimu kwa wawekezaji nchini ni kuwa na mifumo na teknolojia sahihi zinazozingatia afya na usalama wa wafanyakazi,” alisema Mwenda.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, ambaye aliambatana na Naibu Waziri katika ziara hiyo amesema maagizo hayo waliyatoa hivi karibuni wakati Taasisi yake ilipokuwa ikichunguza ajali iliyotokea katika kiwanda cha Fujian Hexingwang ambapo ajali hiyo ilisababisha vifo vya wafanyakazi wawili.
Kwa upande wao wafanyakazi wa kiwanda cha Fujian Hexingwang wameeleza kutofurashwa kwao na jinsi ambavyo mwajiri wao anashindwa kuendesha shughuli zake kwa kuzingatia sheria za nchi.
“Haipendezi kuona mwekezaji kama huyu anakiuka sheria na miongozo mbali mbali anayopewa na mamlaka mbali mbali za serikali jambo ambalo linapelekea hata sisi wafanyakazi kukosa haki zetu za msingi ikiwemo kufanya kazi katika mazingira salama,” alieleza Ramadhani Mdimu.
Ziara hiyo ya Naibu Waziri inafanyika kwa lengo la kufuatilia maboresho yaliyofanyika kufuatia uchunguzi wa ajali zilizotokea katika viwanda viwili vya chuma ambazo zinaonekana zimetokea katika namna inayofanana. Aprili 17 na Mei 04 mwaka huu zilirepotiwa ajali katika kiwanda cha PNP Industries Limited kilichopo Mikocheni ambapo wafanyakazi watatu walijeruhiwa vibaya na nyingine ilitokea katika kiwanda cha Fujian Hexingwang cha Mkuranga ambayo ilipelekea vifo vya wafanyakazi wawili.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment