Serikali Yaongeza Siku Tano Maombi Ya Ajira Za Elimu Na Afya

 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ummy Mwalimu, ametangaza kuongeza muda wa kutuma maombi ya ajira zilizotangazwa na Wizara.

TAMISEMI ilipata kibali cha kuajiri walimu 6,949 na watumishi wa kada mbalimbali za Afya 2,726 ambapo mwisho wa kutuma maombi ulikuwa Mei 23, 2021.

Sasa muda umeongezwa hadi Mei 28, 2021 saa 5:59 usiku, walioshindwa kutuma maombi kwa changamoto yoyote wameshauriwa kufanya hivyo.



from MPEKUZI

Comments