RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa corona ambayo inatarajiwa kutolewa nchini ni hiari na hakuna mtu atakayelazimishwa kufanya hivyo kwa nguvu.
Dk. Mwinyi alisema hayo huko katika Ofisi za Chama Cha Mapindizi (CCM) Mahonda Mkoa wa kaskazini Unguja wakati akizungumza na viongozi wa CCM wa Mmkoa huo katika ziara ya kuwashukuru wananchi na wana CCM wa Mkoa huo baada ya kukichaguwa chama hicho kushika hatamu ya kuongoza dola katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana.
Alisema kuwa Serikali italeta chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa Corona lakini hiyo itakuwa hiari kwa mtu anayehitaji na si lazima kama baadhi ya wananchi wanavyodai kiasi ya kuzusha taharuki.
Alisema chanjo hiyo itatolewa kwa mahujaji wanaotarajiwa kufanya ibada ya Hijja huko Makka, Sauda Arabia ambayo ni sehemu ya masharti ya Serikali hiyo kwa mahujaji watakaotekeleza ibada ya Hijja ili kupunguza uwezekano wa kuibuka kwa mripuko wa maradhi hayo.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment