Samirah Yusuph,
Bariadi. Wananchi wanaoishi maeneo yanayozunguka katika hifadhi ya wanyama pori ya Serengeti wilayani serengeti mkoani Mara wamegeuza changamoto ya uvamizi wa wanyama kuwa fulsa ya kiuchumi ili kukakibilana na wanyama pia kujikwamua kiuchumi.
Wameeleza kuwa mgogoro baina yao na wanyama ni mgogoro ambao utatuzi wake ni mgumu kutoka na kuwa wanachangia mazingira hivyo mwingiliano kati ya shughuli za kibinadamu na wanyama ni mkubwa.
Wameyaeleza hayo walipokuwa katika mafunzo ya ufugaji wa nyuki yaliyotolea na Shirika la Jumuiko la Maliasili Tanzania kwa ushirikiano wa shirika la WWF (world wide fund of nature) yaliyotolewa kwa wananchi 120 kwa lengo la kujifunza jinsi ya kukabiliana na migogoro mbalimbali inayojitokeza katika jamii yaliyo fika tamati leo April 2021, wilayani Bariadi mkoa wa Simiyu.
Ambapo wameeleza kuwa wanyama hasa Tembo wanaovamia katika mashamba yao na kuharibu mazao wamekuwa ninwanyama ambao wanajifunza mazingira hivyo kukwepa mitego na kuendelea kufanya uharibifu.
"Teknolojia ya kutumia mizinga ya nyuki imekuwa na msaada katika kukabiliana wanyama licha ya kuwa tembo wakigundua kama eneo wanalopita lina mizinga ya nyuki wanabadili njia ili kuingia kijijini kufanya uharibifu," alieleza Petronia Wasama mkaza wa Ikona Natta.
"Mbali na kukabiliana na Tembo vile vile ufugaji wa nyuki umekuwa ni fulsa ya ki uchumi kwa sababu Tembo wataogopa nyuki na nyuki hao watatupa asali ambayo itakuwa ni biashara na mazao yataendelea kuwa salama," alieleza Denis Njoroge mkazi wa Makau.
Akielezea mgogoro huo Afisa wanyama pori wilaya ya Serengeti John Meitamei alisema kuwa kwa sasa idadi ya wanyama kuingia katika vijiji imepungua kidogo ikilinganishwa na awali kutokana na kuongezeka kwa teknolojia zinazotumika kuwazuia wanyama kuingia katika makazi.
"Vimeanzishwa vikundi vya vijana ambavyo vimejengewa uwezo wa kulinda wanyama pamoja nakulinda jamii kwa kivuli cha ujasiliamali ambapo vijana watakuwa na fursa za kiuchumi na njia hii imeonyesha matokeo kwa kutumia kauli mbiu ya niwezeshe ili niweze kujilinda na tembo".
Ameongeza kuwa wananchi wenyewe wamekuwa na hamasa kubwa ya kujiunga na vikundi ili kulinda maeneo kwa kupitia mafunzo ambayo wanayapitia licha ya kuwa bado matokeo chanya yanaonekana taratibu lakini mafanikio zaidi ni wananchi kutambua kuwa wanaishi na wanyama na wanyama hawawezi kuondoka hivyo kukubaliana na mazingira.
Akizungumzia namna ambavyo kukubaliana na mazingira ya kuishi na wanyama kwa kujilinda kwa kutumia teknolojia mbali mbali ikiwamo ufugaji wa nyuki Daniel Ouma mratibu wa shirika la Jumuiko na maliasili Tanzania (Tanzania Natural Resources Forum), alisema kuwa lengo ni kutatua migogoro ya wanyapori na binadamu.
"Hatua hiyo itaijengea jamii uwezo wa namna ya kukabiliana na mabadiliko tabia nchi na kutengeneza mpango mkakati kwenye maeneo yao pamoja na Kuwajengea uwezo wa kiuchumu kwa kuwapa jamii mizingira ya kufuga nyuki na namna ya kuandaa mpango biashara".
Mwisho.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment