Rais Samia Afanya Uteuzi Wa Viongozi mbalimbali


 Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali, kwa kumteua Profesa Henry Mahoo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.

Jaji wa Mahakama ya Rufani Dkt. Gerald Ndika yeye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, na ameteuliwa kushika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.

Rais Samia Suluhu Hassan pia amemteua Profesa Aurelia Kamuzora kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa Tanzania.

Profesa Idris Kikula ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini Tanzania, na anashika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.

Aidha, Rais Samia Suluhu Hassan amewateua Profesa Abdulkarim Mruma na Janeth Lekashingo kuwa wajumbe wa Tume ya Madini Tanzania.

Uteuzi wa viongozi hao umeanza tarehe 20 mwezi huu.


from MPEKUZI

Comments