Baraza la kijeshi linalongoza nchi ya Chad kwa kipindi cha mpito limesema halitaingia kwenye mazungumzo na waasi wanaojiita FACT waliokabiliana na wanajeshi wa nchi hiyo wiki moja iliyopita Kaskazini mwa nchi hiyo na kusababisha kifo cha aliyekuwa rais Idriss Deby.
Msemaji wa Baraza hilo la Jeshi Azem Bermandoa Agouna, ametoa kauli hiyo huku akiiomba nchi ya Niger, kusaidia kumkamata kiongozi wa kundi hilo la waasi.
Jumamosi iliyopita, waasi hao walisema wanajiandaa kusitisha mapigano, lakini jeshi nchini Chad linasema lipo kwenye vita na kundi hilo na litaendeleza mashambulizi.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment