Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla amesema kuwa kila mwananchi aliyefika katika Uwanja wa Magufuli wilayani Chato mkoani Geita atapata nafasi ya kupita pembeni ya jeneza lenye mwili wa wa Dkt. John Magufuli kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho.
Amewataka Wananchi kuwa watulivu, kwani hata kama itafika usiku, lakini lazima kila mmoja atapata nafasi ya kuaga.
Ameeleza kuwa, utaratibu uliotumika katika baadhi ya maeneo wa kuzungusha mwili uwanjani mwili wa Dkt Magufuli hautatumika wilayani Chato, na ndiyo sababu walitenga siku moja kwa ajili ya wakazi wa Geita na maeneo jirani.
Akizungumza kuhusu msiba huo, Makamu huyo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla amesema haujaigusa Tanzania pekee bali hata nchi za mbali na Jumuiya ya Kimataifa kutokana na utendaji kazi wa Dkt Magufuli ambao uliwaridhisha wengi.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment